Wednesday, February 18, 2015

Utaratibu wa Kutunuku Matokeo ya Mtihani wa Kidato cha Nne (CSEE) na cha Sita (ACSEE) kwa Kutumia Mfumo wa GPA1     Mfumo wa Wastani wa Pointi (Grade Point Average GPA)
·         Huonesha wastani wa pointi alizopata mtahiniwa katika masomo aliyofaulu katika mtihani wake.

·         GPA hutokana na masomo  saba (07) aliyofaulu vizuri zaidi mtahiniwa katika Mtihani wa Kidato cha Nne na masomo  matatu (03) ya tahasusi katika Mtihani wa Kidato cha Sita. Mtahiniwa aliyefanya masomo pungufu ya 07 kwa CSEE au pungufu ya 03  kwa ACSEE, atafaulu katika kiwango cha “Pass” endapo atapata angalau Gredi D katika masomo mawili au gredi C, B, B+ au A katika somo moja.

·          Uzito wa Gredi A= 5, B+ = 4, B = 3, C = 2, D = 1, E = 0.5 na F = 0.


2   Ukokotoaji wa GPA ya Mtahiniwa
·         Hufanyika kwa kuchukua jumla ya uzito wa gredi katika masomo saba (07) aliofanya vizuri kwa Mtihani wa Kidato cha Nne na matatu  (03) ya tahasusi kwa Mtihani wa Kidato cha Sita na kugawanya kwa idadi ya masomo. Ukokotoaji huo huzingatia kanuni ifuatayo:

GPA =    Jumla ya Uzito wa gredi za masomo
               ------------------------------------------------
               Idadi ya Masomo

·         Masomo yatakayotumika katika ukokotoaji wa GPA ya mtahiniwa ni yale ambayo amefaulu; yaani amepata Gredi A, B+, B, C au D.

Muundo wa Madaraja Kwa Kutumia Mfumo wa GPA
·         Katika mfumo wa Wastani wa Pointi (GPA) kutakuwa na madaraja manne ambayo ni  Distinction, Merit, Credit na Pass.

Daraja la juu la ufaulu ni  Distinction na la chini ni  Pass kama ilivyoainishwa katika Jedwali lifuatalo:
DARAJA
CSEE
(Kidato cha Nne)
ACSEE
(Kidato cha Sita)
DARAJA KWA ZAMANI

Distinction

3.6 – 5.0

3.7 – 5.0

Daraja la  I


Merit


2.6 – 3.5


3.0 – 3.6


Daraja la  II

Credit


1.6 – 2.5


1.7 – 2.9


Daraja la  III
Pass

0.3 – 1.5

0.7 – 1.6

               Daraja la  IV
Fail
0.0 – 0.2
0.0 – 0.6
Daraja la  0


MFANO;
Mtihani wa Kidato cha Nne, mtahiniwa aliyepata ufaulu wa Civics (A), History (B+), Geography (B+), Kiswahili (B),  English (C), Physics (C), Chemistry (C), Biology (C) na Mathematics (E) atakuwa na jumla ya pointi 22 kwenye masomo saba  aliyofanya vizuri.
Idadi hiyo ya pointi ikigawanywa kwa idadi ya masomo saba (07), Mtahiniwa huyu atakuwa na Wastani wa  Pointi (GPA) 3.1 na atatunukiwa daraja la  Merit.

Civics (A) = 5;
History (B+) = 4;
Geography (B+) =4;
Kiswahili (B) =3;
English (C) =2;
Physics (C) =2;
Chemistry (C) =2;
Biology (C) =2;
Mathematics (E) =0.5;

Masomo saba aliyofaulu zaidi Civics, History, Goegraphy, Kiswahili, English, Physics na Chemisrty:
GPA = 5+4+4+3+2+2+2 
                        7
 GPA =  22
               7
GPA = 3.14285 ;  

GPA = 3.1 ;  
Mtahiniwa atakua amepata daraja la MERIT ambalo ni sawa na DARAJA LA PILI.


Katika Mtihani wa Kidato cha Sita mtahiniwa aliyepata ufaulu wa Physics (A), Chemistry (B+), Biology (A), Basic Applied Mathematics (D) na General Study (A) atakuwa na jumla ya pointi 14 kwenye  masomo ya tahasusi (PCB). Idadi hiyo ya pointi ikigawanywa kwa idadi ya masomo matatu (03), mtahiniwa atakuwa na Wastani wa Pointi (GPA) 4.7 na atatunukiwa daraja la Distinction.

Physics (A) = 5;
Chemistry (B+) = 4;
Biology (A) = 5;
Basic Applied Mathematics (D) = 1;
General Study (A) = 5;

Masomo Tahasusi (Combination ya mtahiniwa) Physics, Chemistry na Biology.
GPA = 5+4+5
               3
GPA = 14 
             3
GPA = 4.6666

GPA = 4.7
Mtahiniwa atakua amepata daraja la DISTINCTION ambalo ni sawa na DARAJA LA KWANZA.

Angalia Matokeo ya kidato cha  nne 2014


Maelezo zaidi kuhusu GPA yanapatikana katika tovuti ya Baraza la Mitihani (www.necta.go.tz).

Tuesday, July 22, 2014

Haya ndio Madaraja mapya ya matokeo ya kidato cha sita 2014

Kuna alama aina saba yani A, B+, B, C, D, E na F. 

(i)  A ni Ufauli Uliojipambanua;

(ii) B+ ni Ufaulu bora sana;

(iii) B ni 
Ufaulu mzuri sana;

(iv)C ni Ufaulu mzuri;

(v) D ni Ufaulu Hafifu

(vi) E ni 
Ufaulu hafifu sana na

(vii)  F ni 
Ufaulu usioridhisha


Kulingana huu muundo mpya wa alama, uwigo wake ni kama ifuatavyo;
A 75 - 100

B+ 60 - 74
B 50- 59
C 40 - 49
D 30 - 39
E 20 - 29
F 0 - 19 


Na mfumo mpya wa madaraja ni:
3 - 7 I Ufauli Uliojipambanua

8 - 9 II Ufaulu bora sana 

10 - 13 III Ufaulu mzuri

14 - 16 IV Ufaulu Hafifu 

17 - 21 O Ufaulu usioridhisha.

Kwa kukokotoa madaraja na pointi:
A ni1,
B+ ni 2,
B ni 3,
C ni 4,
D ni 5, 
E ni 6  and
Fni 7.

Jumla ya pointi inapatikana kwa kujumlisha masomo matatu(3) yenye ufaulu bora zaidi isipokua masomo madogo(subsidiary subject) mfano General Studies na BAM.

New NECTA grades system used in Form Six Examination Results 2014

There are seven grades indicated as A, B+, B, C, D, E, and F. 

(i)  A is distinction or outstanding performance

(ii) B+ is excellent performance

(iii) B is very good performance;

(iv)C is good performance;

(v) D is low performance

(vi) E is very low performance and

(vii)  F is unsatisfactory performance.According to these new grades;
A 75 - 100

B+ 60 - 74
B 50- 59
C 40 - 49
D 30 - 39
E 20 - 29
F 0 - 19 


And new division system is:
3 - 7 I 
Outstanding performance 

8 - 9 II Excellent performance 

10 - 13 III Good performance 

14 - 16 IV Low performance 

17 - 21 O Unsatisfactory performance.

To calculate the division and points.
A is 1,
B+ is  2,
B is 3,
C is 4,
D is 5, 
E is 6  and
F is 7.

Total points obtained by adding 3  best performed subjects except the subsidiary subjects.