1 Mfumo
wa Wastani wa Pointi (Grade Point Average GPA)
·
Huonesha wastani wa pointi alizopata
mtahiniwa katika masomo aliyofaulu katika mtihani wake.
·
GPA hutokana na masomo saba (07) aliyofaulu vizuri zaidi mtahiniwa
katika Mtihani wa Kidato cha Nne na masomo
matatu (03) ya tahasusi katika Mtihani wa Kidato cha Sita. Mtahiniwa aliyefanya
masomo pungufu ya 07 kwa CSEE au pungufu ya 03
kwa ACSEE, atafaulu katika kiwango cha “Pass” endapo atapata angalau
Gredi D katika masomo mawili au gredi C, B, B+ au A katika somo moja.
·
Uzito wa Gredi A= 5, B+ = 4, B = 3, C = 2, D =
1, E = 0.5 na F = 0.
2 Ukokotoaji wa GPA ya Mtahiniwa
·
Hufanyika kwa kuchukua jumla ya uzito
wa gredi katika masomo saba (07) aliofanya vizuri kwa Mtihani wa Kidato cha Nne
na matatu (03) ya tahasusi kwa Mtihani wa
Kidato cha Sita na kugawanya kwa idadi ya masomo. Ukokotoaji huo huzingatia kanuni
ifuatayo:
GPA = Jumla ya
Uzito wa gredi za masomo
------------------------------------------------
Idadi
ya Masomo
·
Masomo yatakayotumika katika ukokotoaji
wa GPA ya mtahiniwa ni yale ambayo amefaulu; yaani amepata Gredi A, B+, B, C au
D.
3 Muundo wa Madaraja Kwa Kutumia Mfumo
wa GPA
·
Katika mfumo wa Wastani wa Pointi (GPA)
kutakuwa na madaraja manne ambayo ni Distinction,
Merit, Credit na Pass.
Daraja la juu la ufaulu ni Distinction na la chini ni Pass kama ilivyoainishwa katika Jedwali
lifuatalo:
DARAJA
|
CSEE
(Kidato cha Nne)
|
ACSEE
(Kidato cha Sita)
|
DARAJA KWA ZAMANI
|
Distinction
|
3.6
– 5.0
|
3.7
– 5.0
|
Daraja la I
|
Merit
|
2.6
– 3.5
|
3.0
– 3.6
|
Daraja la II
|
Credit
|
1.6
– 2.5
|
1.7
– 2.9
|
Daraja la III
|
Pass
|
0.3
– 1.5
|
0.7
– 1.6
|
Daraja la IV
|
Fail
|
0.0
– 0.2
|
0.0
– 0.6
|
Daraja
la 0
|
MFANO;
Mtihani wa Kidato cha Nne,
mtahiniwa aliyepata ufaulu wa Civics (A), History (B+), Geography (B+), Kiswahili
(B), English (C), Physics (C), Chemistry
(C), Biology (C) na Mathematics (E) atakuwa na jumla ya pointi 22 kwenye masomo
saba aliyofanya vizuri.
Idadi hiyo ya pointi ikigawanywa kwa idadi ya masomo saba (07),
Mtahiniwa huyu atakuwa na Wastani wa Pointi
(GPA) 3.1 na atatunukiwa daraja la Merit.
Civics (A) = 5;
History (B+) = 4;
Geography (B+) =4;
Kiswahili (B) =3;
English (C) =2;
Physics (C) =2;
Chemistry (C) =2;
Biology (C) =2;
Mathematics (E) =0.5;
Masomo saba aliyofaulu zaidi Civics, History, Goegraphy, Kiswahili, English, Physics na Chemisrty:
GPA = 5+4+4+3+2+2+2
7
GPA = 22
7
GPA = 3.14285 ;
GPA = 3.1 ;
Mtahiniwa atakua amepata daraja la
MERIT ambalo ni sawa na DARAJA LA PILI.
Katika Mtihani wa Kidato cha Sita
mtahiniwa aliyepata ufaulu wa Physics (A), Chemistry (B+), Biology (A), Basic Applied
Mathematics (D) na General Study (A) atakuwa na jumla ya pointi 14 kwenye masomo ya tahasusi (PCB). Idadi hiyo ya pointi
ikigawanywa kwa idadi ya masomo matatu (03), mtahiniwa atakuwa na Wastani wa
Pointi (GPA) 4.7 na atatunukiwa daraja la Distinction.
Physics (A) = 5;
Chemistry (B+) = 4;
Biology (A) = 5;
Basic Applied Mathematics (D) = 1;
General Study (A) = 5;
Masomo Tahasusi (Combination ya mtahiniwa) Physics, Chemistry na Biology.
GPA = 5+4+5
3
GPA = 14
3
GPA = 4.6666
GPA = 4.7
Mtahiniwa atakua amepata daraja la DISTINCTION
ambalo ni sawa na DARAJA LA KWANZA.
Angalia Matokeo ya kidato cha nne 2014
Maelezo zaidi kuhusu GPA yanapatikana katika tovuti ya
Baraza la Mitihani (www.necta.go.tz).
0 comments:
Post a Comment