Wednesday, February 18, 2015

Utaratibu wa Kutunuku Matokeo ya Mtihani wa Kidato cha Nne (CSEE) na cha Sita (ACSEE) kwa Kutumia Mfumo wa GPA



1     Mfumo wa Wastani wa Pointi (Grade Point Average GPA)
·         Huonesha wastani wa pointi alizopata mtahiniwa katika masomo aliyofaulu katika mtihani wake.

·         GPA hutokana na masomo  saba (07) aliyofaulu vizuri zaidi mtahiniwa katika Mtihani wa Kidato cha Nne na masomo  matatu (03) ya tahasusi katika Mtihani wa Kidato cha Sita. Mtahiniwa aliyefanya masomo pungufu ya 07 kwa CSEE au pungufu ya 03  kwa ACSEE, atafaulu katika kiwango cha “Pass” endapo atapata angalau Gredi D katika masomo mawili au gredi C, B, B+ au A katika somo moja.

·          Uzito wa Gredi A= 5, B+ = 4, B = 3, C = 2, D = 1, E = 0.5 na F = 0.


2   Ukokotoaji wa GPA ya Mtahiniwa
·         Hufanyika kwa kuchukua jumla ya uzito wa gredi katika masomo saba (07) aliofanya vizuri kwa Mtihani wa Kidato cha Nne na matatu  (03) ya tahasusi kwa Mtihani wa Kidato cha Sita na kugawanya kwa idadi ya masomo. Ukokotoaji huo huzingatia kanuni ifuatayo:

GPA =    Jumla ya Uzito wa gredi za masomo
               ------------------------------------------------
               Idadi ya Masomo

·         Masomo yatakayotumika katika ukokotoaji wa GPA ya mtahiniwa ni yale ambayo amefaulu; yaani amepata Gredi A, B+, B, C au D.

Muundo wa Madaraja Kwa Kutumia Mfumo wa GPA
·         Katika mfumo wa Wastani wa Pointi (GPA) kutakuwa na madaraja manne ambayo ni  Distinction, Merit, Credit na Pass.

Daraja la juu la ufaulu ni  Distinction na la chini ni  Pass kama ilivyoainishwa katika Jedwali lifuatalo:
DARAJA
CSEE
(Kidato cha Nne)
ACSEE
(Kidato cha Sita)
DARAJA KWA ZAMANI

Distinction

3.6 – 5.0

3.7 – 5.0

Daraja la  I


Merit


2.6 – 3.5


3.0 – 3.6


Daraja la  II

Credit


1.6 – 2.5


1.7 – 2.9


Daraja la  III
Pass

0.3 – 1.5

0.7 – 1.6

               Daraja la  IV
Fail
0.0 – 0.2
0.0 – 0.6
Daraja la  0


MFANO;
Mtihani wa Kidato cha Nne, mtahiniwa aliyepata ufaulu wa Civics (A), History (B+), Geography (B+), Kiswahili (B),  English (C), Physics (C), Chemistry (C), Biology (C) na Mathematics (E) atakuwa na jumla ya pointi 22 kwenye masomo saba  aliyofanya vizuri.
Idadi hiyo ya pointi ikigawanywa kwa idadi ya masomo saba (07), Mtahiniwa huyu atakuwa na Wastani wa  Pointi (GPA) 3.1 na atatunukiwa daraja la  Merit.

Civics (A) = 5;
History (B+) = 4;
Geography (B+) =4;
Kiswahili (B) =3;
English (C) =2;
Physics (C) =2;
Chemistry (C) =2;
Biology (C) =2;
Mathematics (E) =0.5;

Masomo saba aliyofaulu zaidi Civics, History, Goegraphy, Kiswahili, English, Physics na Chemisrty:
GPA = 5+4+4+3+2+2+2 
                        7
 GPA =  22
               7
GPA = 3.14285 ;  

GPA = 3.1 ;  
Mtahiniwa atakua amepata daraja la MERIT ambalo ni sawa na DARAJA LA PILI.


Katika Mtihani wa Kidato cha Sita mtahiniwa aliyepata ufaulu wa Physics (A), Chemistry (B+), Biology (A), Basic Applied Mathematics (D) na General Study (A) atakuwa na jumla ya pointi 14 kwenye  masomo ya tahasusi (PCB). Idadi hiyo ya pointi ikigawanywa kwa idadi ya masomo matatu (03), mtahiniwa atakuwa na Wastani wa Pointi (GPA) 4.7 na atatunukiwa daraja la Distinction.

Physics (A) = 5;
Chemistry (B+) = 4;
Biology (A) = 5;
Basic Applied Mathematics (D) = 1;
General Study (A) = 5;

Masomo Tahasusi (Combination ya mtahiniwa) Physics, Chemistry na Biology.
GPA = 5+4+5
               3
GPA = 14 
             3
GPA = 4.6666

GPA = 4.7
Mtahiniwa atakua amepata daraja la DISTINCTION ambalo ni sawa na DARAJA LA KWANZA.

Angalia Matokeo ya kidato cha  nne 2014


Maelezo zaidi kuhusu GPA yanapatikana katika tovuti ya Baraza la Mitihani (www.necta.go.tz).


0 comments:

Post a Comment